Jinsi ya kupakua toleo la PDF la kamusi hii

 

Screenshot

Unapobonyeza Pakua kwenye menyu ya juu, wewe huweza kupakua toleo la PDF la kamusi hii. Toleo la aina hii linakuwezesha kusoma kamusi katika kompyuta yako jinsi unavyosoma toleo linalochapishwa kwenye karatasi. Linafanana kamili na toleo linalochapishwa kwenye karatasi lakini liko katika muundo wa kielektroniki. Mara tu baada ya kupakua, huweza kusoma kamusi bila kuunganishwa na mtandao.

Pia inawezekana kuchapisha sehemu za kamusi ukiwa na mtambo wa kuchapishia (kama vile printa).