Dibaji

 

Kikabwa ni lugha katika eneo la Mashariki la lugha za Kibantu. Kinazungumzwa na watu mnamo 14,000 wanaoishi kilomita kadhaa kutoka Ghuba la Mara la Ziwa Victoria, Kaskazini mwa Tanzania. Wakabwa wanaishi katika wodi ya Bukabwa, tarafa ya Makongoro, wilaya ya Butiama, mkoani mwa Mara.

 

Kikabwa kinaainishwa katika Ethnologue kuwa lugha ya Niger-Congo, Atlantic-Congo, Volta-Congo, Benue-Congo, Bantoid, Southern, Narrow Bantu, Central, J, Logooli-Kuria (E.405). Wakabwa wanaita lugha yao "Ekikabhwa" na katika kiingereza kinaitwa "Kabwa." Maneno ya Kikabwa yanafanana na lugha tatu zingine kwa asilimia kubwa: Kisweta (86%), Kikiroba (80%), na Kikuria (73%).